Kwa mujibu wa S Shirika la Habari la Hawza, Ayatollah Ali Khamenei ametoa jibu la swali kuhusu "kile kilichosalia katika wosia wa mali ya maiti" jawabu ambalo linawasilishwa kwenu kama ifuatavyo.
Kile kilichosalia katika wosia wa mali ya maiti
Swali:
Mtu anamkabidhi mwenzake kiasi cha fedha kama amana, kwa sharti kwamba baada ya kifo chake zitumike kwa ajili ya gharama za mazishi na sanda, kuswaliwa kwa muda maalumu, kufungiwa saumu, kulipa haki za watu (raddi madh'alim) na kuandaa vikao vya khitma. Ikiwa baada ya kutekeleza mambo yaliyotajwa fedha zitabaki, je, kiasi hicho kilichosalia ni mali ya warithi au kinapaswa kutumika kwa mambo ya kheri?
Jawabu:
Iwapo baada ya kutoa madeni na wajibu wa kifedha wa maiti, jumla ya mali iliyowekwa amana haitazidi theluthi moja ya mali yote ya maiti, basi kiasi kilichosalia kitumike kwa ajili ya kulipa haki za watu (raddi madhalim).
Maoni yako